Sunday, December 2, 2012

WANAUME 5,838 WAFANYIWA TOHARA MKOANI TABORA


 
Na Lucas Raphael,Sikonge

Tohara ya Wanaume.Baada ya upasuaj
JUMLA ya wanaume 5,838 mkoani Tabora wamefanyiwa Tohara  katika kampeni maalum inayondeshwa na asasi ya kiraia ,kupitia wizara ya afya na ustwi wa jamii,ikiwa na lengo la kupunguza kasi ya maambukizi ya ukimwi kwa wanaume.

MBOO AMBAYO AJIFANYIWA TOHARA
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Tabora ,Fatuma Mwassa wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yaliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Tasaf wilayani Sikonge mkoani hapa.

Alisema kwamba kampeni hiyo ya Tohara kwa wanaume inaweza kupunguza kasi ya maambukizi kwa kundi mmoja la wanaume, kwani kwa kufanya hivyo tayari watakuwa wameokoa maisha ya kundi lingine la wanawake.

Alisema kuwa licha ya kufanyika kwa tohara bado kampeni hiyo inaendelea katika wilaya zote za mkoa wa Tabora kwa lengo la kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wanaume wote wenye tatizo hilo.

Mwassa alisema katika kipindi cha januari mwaka huu hadi septemba jumla ya watu 41,032 walipima afya zao kati ya hao wananume walikuwa ni 19,531 na wanawake walikuwa 21 591 waliokutwa na maambukizi ni 3,136 ni wanaume na wananwake ni 1,812 sawa na asilimia 7.6

Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa wa tabora akizungumzia changamoto mbalilmbali zinaukabili mkoa huu alisema kwamba ugonjwa wa ukimwi ni kuongezeka kwa idadi ya watoto yatima na waishio katika mazingira magumu.

Awali afisa uhamasishaji  na usambazaji wa PSI mkoani tabora ,Gabriel Setumbi alimwambia mkuu huyo wa mkoa kuwa kwa kipindi cha januari hadi novemba mwaka huu wameweza kusambaza mipira ya kikie na kiume kiasi cha pakiti 1,618,704 ambayo ni sawa na katoni 3747 ambapo mipira ya kike ni pakiti 57,600 sawa na katoni 320.

Aidha alisema kwamba Psi wamekuwa wakielimisha jamii juu ya matumizi sahihi ya kondom kwa kupitia kwa njia ya sinema ambao hutoa ujumbe juu namna ya kujikinga na kujiepusha na mambukizi ya ukimwi .

Setumbi aliendelea kusema kwamba asasi hiyo imeweza kutembelea wilaya zote za mkoa wa tabora na takribani maeneo 65 ya vijijini na kata mbalimbali wameyafikia na kutoa elimu ya ukimwi.

Mwisho

No comments:

Post a Comment