Wednesday, October 17, 2012

ALBINO WAPATI NG'OMBE



Na Lucas Raphael,Tabora

WATANZANIA wanaoishi Nchini Uingereza wameamua kuapatia mradi wa Ng'ombe wa maziwa wanawake wenye ulemavu wa ngozi,albino,wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni kumi za Kitanzania.

Katibu wa Chama cha Maalbino,Mkoani Tabora.Musa Kabimba alisema mradi huo umetolewa kwa wanawake albino wapatao thelathini na sita kutoka wilaya zote za Mkoa wa Tabora.

Alisema jumla ya Ng'ombe wa maziwa hamsini wametolewa kwa wanawake hao ukiwa ni mchango kutoka kwa watanzania wanaoishi Nchini Uingereza wakiwa na chama chao kinachojulikana kwa jina la Tanzania Development Trust,TDT kinachoongozwa na mwenyekiti wake Julian Marcus.

Kabimba ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha maalbino Nchini,alisema mradi huo umekuja wakati wana uhitaji mkubwa kwa wanawake wenye ulemavu wa ngozi Mkoani Tabora kwa vile wana hali ngumu sana  kimaisha ukilinganisha na wanaume wenye ulemavu wa ngozi ingawa nao alisema wana hali mbaya pia.

Alisema maziwa ya ng'ombe kila siku yatauzwa na pesa yake kutumiwa na wanawake wenye ulemavu wa ngozi kujikimu kimaisha na kuanzisha miradi ya kiuchumi ambayo itawaongezea zaidi kipato chao.

Katika mradi huo ng'ombe jike watakaozaliwa watapewa moja kwa moja wanawake wenye ulemavu wa ngozi na kama akizaliwa Ng'ombe dume atauzwa na pesa yake kutunisha mfuko wa wanawake hao katika wilaya husika.

Alibainisha kwamba mradi huo utasimamiwa na chama cha maalbino mkoa wa Tabora na utahusisha wilaya zote za Mkoa wa Tabora.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment