Sunday, October 28, 2012

MABINGWA WA BALIMI BOAT RACE KAGERA WAPATIKANA



 Katibu Tawala wa Manispaa ya Bukoba Clement Ndiomukama, akimkabidhi kitita cha Tsh.900,000 Nahodha wa timu ya Kabanga Bushasha, Eliudi Prospa baada ya kuibuka mabingwa kwenye mashindano ya (Mitumbwi)  Balimi Boat Race Wilayani Bukoba Mkoani Kagera jana ambapo washiriki walishindana kuendesha  mitumbwi kwa makasia.
 Mabingwa wa mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) Mkoani Kagera  upande wa wanaume timu ya Kabanga Bushasha wanaume wakishangilia mara baada ya kuwa mabingwa wa mkoa huo na kukabidhiwa jumla ya shilingi laki tisa (900,000) kama zawadi ya ushindi wa kwanza.
 Mabingwa wa mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) Mkoa wa Kagera upande wa wanawake Timu ya Seleka kutoka Musila, wakishangilia mara baada ya kuwa mabingwa wa mkoa huo na kukabidhiwa jumla ya shilingi laki saba (700,000) kama zawadi ya ushindi wa kwanza.
 Katibu tawala wa Manispaa ya Bukoba Clement Ndiamukama, akifungua mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) yaliyofanyika Wilayani Bukoba Mkoani Kagera ambapo zaaidi ya timu 50 zenye watu watano kila timu zilishiriki, ambapo walishindana kupiga kasia kwa umbali wa Kilometa 3 kwenda na kurudi, kushoto ni Meneja wa Mauzo wa Kanda ya Ziwa Endrew Mbwambo na Afisa wa Sumatra Kapteni Alex Katama.
 Meneja wa Bia ya Balimi Edith Bebwa(kulia) akizungumza na washiriki wa mashindano ya Balimi Boat Race Wilayani Bukoba Mkoani Kagera mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo ambapo timu tano zitakwenda kuwakilisha mkoa huo kwenye fainali zitakazofanyika mkoani Mwanza Disemba mwaka huu.
 Waokoaji wakiwakoa wapiga kasia kinamama ambao walipinduka
Mabingwa Wanaumr Wakishangilia Baada Ya Kuwasili


WASHIRIKI wa shindano la mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) ambayo ni maalum kwa mikoa ya kanda ya ziwa wametakiwa kutumia pesa wanazozipata kwaajili ya kujiendeleza kwenye miradi ya maendeleo.
 
Akizungumza mara baada ya mashindano hayo Meneja wa Kinywaji hicho Cha Balimi Edith Bebwa, alisema lengo la mashindano hayo ni kutoa shukrani na kuwawezesha wanywaji wake hivyo wanapaswa kuzitumia kwenye kujiendeleza kwenye miradi yao.
 
“Nawaomba mlioshinda na washiriki wengine ambao pia mmepata pesa hizo mzitumie kwenye miradi yenu kama ni mvuvi basi ongeza chombo kingine au nyavu ili mradi uzitumie kwenye uzalishaji” alisema Bebwa.
 
Awali akifungua mashindano hayo Katibu Tawala wa Manispaa ya Bukoba Clement Ndiamukama aliwataka washiriki watakaoshinda kutobweteka na ubingwa badalayake wajipange kwa mazoezi ili kwenye fainali ya mashindano hayo waupe heshima Mkoa wa Kagera.
 
“Tunataka mtuletee heshima kwahiyo wale watakaoshinda watambue wajibu huo wakuletea heshima Mkoa,” alisema Ndiomukama.
 
Mashindano hayo ambayo yalianza Mkoani Kigoma October 27 mwaka huu yanatarajiwa kumalizika kwenye fainali zitakazofanyika mwezi Disemba mwaka huu Mkoani Mwanza.

No comments:

Post a Comment