Wednesday, October 24, 2012

KIONGOZI WA UAMSHO HII ISHARA YAKO INATUCHANGANYA!!!!

 : 


Kiongozi wa uamsho Zanzibar 
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kwa baadhi ya watu waliohudhuria mahakamani na hata wale wanaoperuzi kwenye mitandao wamebahatika kumuona kiongozi huyu wa kundi la Uamsho akitoa Ishara hii wakati akiteremka kwenye gari la Polisi mara baada ya kufikishwa mahakamani kufuatia kesi inayomkabiri.
 
Kumekuwepo hali ya kujiuliza kuhusu Ishara hizi ambazo kama ilivyozoeleka hapa nchini hutumiwa na Chama fulani cha kisiasa kama sehemu na nembo za utambulisho unaoeleweka na kukubalika kisheria.
 
Baadhi ya watu wamekuwa wakijiuliza hivi hapa kuna utetezi wa maslahi ya kidini kweli au ni ya Chama?...au ni mchanganyiko katika kuhakikisha kile kinachodaiwa kuwa kutafuta haki hata kwa ncha ya upanga?
 
Najaribu kuangalia,na kama nitakuwa sahihi naomba viongozi wa dini na wale wenye ujuzi ya mambo ya dini waweze kunisadia,...Hivi kwenye dini ya kiislamu hii ni Ishara gani?....na kama inakosekana kwenye dini ya kiislamu,kwakuwa mimi ni mtanzania hapa nitakuwa naelewa kuwa kiongozi huyu wa dini ya kiislamu najua atakuwa anamuelekeo wa Chama fulani cha kisiasa kilichopo hapa nchini.
 
Kwaupande mwingine kama kiongozi huyu angekuwa akinisikia na pengine kuona hiki ninachokiandika hapa angeweza kuniambia kama kweli hakuna mkono wa mtu juu ya madai hayo waliyonayo kupitia kivuli cha dini.
 
Natambua kuwa mvutano huu umesababisha kwa kiasi kikubwa mgawanyiko kwani wapo waislamu wanaunga mkono na wapo ambao wanapingana na yote hayo na pengine kuona kuwa huo ni uvunjifu wa amani nchini.

Binafsi nachukua nafasi hii pamoja na yote hayo yanayoendelea kujitokeza na kutishia amani ya nchi namuomba kiongozi huyu wa dini ya kiislamu anifafanulie hii Ishara aliyoionesha wakati anafikishwa mahakamani ina maana gani?....SAMAHANI LAKINI.     

No comments:

Post a Comment