Sunday, October 21, 2012

WANANCHI WATAKA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA


BAADHI ya wananchi wa kata ya tutuo na sikonge mjini wilayani sikonge mkoani Tabora wamesema kuwa katiba mpya ijayo iwe ya serikali ya umoja wa kitaifa kulingana na mfumo wa vyama vingi uliopo hivi sasa.

Wakitoa maoni ya mabadiliko ya katiba mpya wakati tume hiyo ilipo tembelea kata hizo kwa nyakati tofauti wilayani hapa walisema kuwa katiba ijayo iwe na serikali ya umoja wa kitaifa kutokana na mfumo wa vyama vingi vilivyopo hapa nchini.

Walisema kuwa mfumo wa vyama vingi vya siasa  unapaswa kuwa na serikali ya umoja wa kitaifa ili dhana hiyo ya vyama vingi iweze kutimia pamoja na kuepusha machafuko yanayo weza kujitokeza.

Walisema nchi zilizo endelea ambazo zinajali mfumo huo wa vyama mvingi vinatumia mfumo huo wa serikali ya umoja wa kitaifa katika kuendesha shuguli zote za kiserikali.

Sabina kiwinga mkazi wa kata ya tutuo alisema kuwa serikali ya umoja wa kitaifa italeta sura mpya katika katiba endepo pendekezo hilo litakubaliwa na kufanyiwa kazi.

Alisema kuwa utawala huo utaongeza wigo wa viongozi bora kutoka vyama mbalimbali tofauti na sasa baadhi ya viongozi hawatendi haki kwa wananchi wao.

Alisema kuwa serikali hiyo ya umoja wa kitaifa itatoa fursa ya kusikiliza kero za wananchi bila kujali itikadi za dini wala kisiasa pamoja na kuhakikisha sheria za nchi zinalindwa kwa kufuata taratibu na kanuni ya katiba hiyo itakayo pendekeza.

Wananchi hao wakifafanua serikali hiyo ya umoja wa kitaifa itakavyo kuwa ni chama kitakacho pata kura nyingi kitapata kiti cha urais,makamu wa kweanza wa rais atatoka chama pinzani ambapo makamu wa pili wa rais atatoka chama tawala.

Wakipanga kazi za viongozi hao kwanayakati mbalimbali wananchi hao walisema kuwa makamu wa kwanza wa rais atapangiwa wizara maalumu za kufanyia kazi pamoja na kuwa mshauri wa rais huku makamu wa pili wa rais atakuwa mtendaji mkuu wa serikali.

Hirida kamba alisema kuwa mawaziri na rais wote katika katiba itakayoyo undwa mishahara yao wote iwe hadharani ili kila mwananchi aweze kufahamu tofauti na sasa mishahara hiyo haifahamiki kwa wananchi hao.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment