Tuesday, October 16, 2012

DC KUMCHAYA AHIMIZA KUTUNZA NA KUENZI KUMBUKUMBU ZA MWALIMU NYERERE


 Mkuu wa wilaya ya Tabora Bw.Suleiman Kumchaya akiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na wa kamati ya Sherehe ya  maadhinisho ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere mjini Tabora katika picha ya pamoja Shule ya Sekondari Tabora wavulana ambako Mwl.Nyerere alianza kupata elimu mnamo mwaka 1937 - 1942.
 Mnara wa kumbukumbu ya Uamuzi wa busara Tabora ulioko soko kuu mjini humo.
 Wakiangalia kumbukumbu mbalimbali za Mwl.Nyerere kwa lengo la kumuenzi eneo la Taasisi mjini Tabora lililotumika kufanyia mikutano ya kudai uhuru wa Tanganyika.
 Mkuu wa wilaya ya Tabora Bw.Suleimani Kumchaya akipaka rangi eneo la kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Taasisi mjini Tabora.
 Mkuu wa wilaya akiwa na wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama wilaya ya Tabora na wa kamati ya Sherehe ya maadhimisho ya siku ya kumkumbuka Mwalimu Nyerere,katika maandamano mjini Tabora wakimuenzi mwalimu JK Nyerere. 
 Mmoja kati ya walimu wa Sekondari ya Tabora Wavulana Bw.Charles Lihembepahi akionesha ramani iliyokuwa ikionesha harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika katika Jengo la kumbukumbu ya mwalimu Nyerere Shuleni hapo.
 Baadhi ya picha zilizopo katika Jengo hilo zilizopigwa enzi ya Mwalimu Nyerere.
 Baadhi ya wadau wakisoma machapisho ya kumbukumbu za Mwalimu Nyerere.

Kikundi cha Sanaa cha JKT Tabora kikitumbuiza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika Taasisi mjini Tabora.

No comments:

Post a Comment