Saturday, October 20, 2012

KATIBA MPYA IFUTE KODI ZA PIKIPIKI .


   





Na Lucas Raphael,Sikonge
.
WANANCHI wa kata ya ipole na kitunda wilayani sikonge mkoani Tabora  wamesema katiba mpya itakayoundwa ifute kodi za pikipikpi kutokana na usafiri huo kuwa ni rahisi vijijini katika kutoa huduma mbalimbali kwa jamii hiyo.

Wakitoa maoni ya mabadiliko ya katiba mpya wakati tume hiyo ilipo tembelea kata hizo kwa nyakati tofauti wilayani hapa walisema kuwa usafiri huo utolewe uwe kama usafiri wa Baiskeli ambao hauna kodi za shurti kama pikipiki. 

Walisema baadhi ya Askari polisi wilayani humo huwa shurutisha wananchi hao wakati wa kukamata kodi hali ambayo baadhi ya wakazi hao hushindwa kumudu ghalama hizo.

Walisema kuwa Askari hao huwafukuza wananchi kwa pikipiki ili wapate kodi hiyo na kama wananchi huyo hana kodi hunyanganywa pikipiki hiyo mpaka alipe kodi hiyo.

Walibainisha kodi za kero ambazo wanapendekeza zifutwe ili usafiri huo uwe kama Baiskeli ni pamoja na kodi ya Leseni ya udreva Daraja (A),Bima,sitika za ya ukaguzi pamoja na kofia(helment).

Walisema kero hizo zimewasukuma kudai katiba itakayo uindwa pikipiki iwe huru kama baiskeli ilikodi za kero katika usafiri huo zifutwe pamoja na kuondokana na kukimbizana na Askari polisi ambao wame kuwa kero kwa wananchi hao kutokana na kukamatwa kwa vyombo vyao.

’’Maoni yetu ni kwamba pikipiki iwe huru kama Baiskeli kodi zake zote zifutwe kwani ndio usafiri wetu waharaka sisi wananchi wa vijijini pamoja na kupunguza kero ya polisi wetu ambao tunakimbizana mitaani kwa kudai kodi ambazo hata faida pengine hazina katika pato la ndani’’alisema mkazi mmoja wa ipole. 

Sophia Maganga (63) mkazi wa kata ya kitunda akichangia maon hayo kwan iaba ya wanawake wa kata hiyo ambaye alijitokeza pekee alisema kuwa usafiri huo unawasaidia wanawake hususani wakati wa kujifungua pamoja na maeneo mengi ya vijijini kukosa usafiri mwingine zaidi ya huo.

Sophia alisema kuwa katiba mpya itakayopendekezwa ihakikishe kodi za shurti za pikipiki zifutwe ili wananchi waweze kunufaika na usafiri huo pamoja na kupunguza kero za polisi na maofisa wa T R A. 

’’kama kweli mme kuja kupata maoni yetu mimi kama mwanamke pekee niliyeongea katika kikao hiki tunaomba kodi zote zifutwe ili wananchi tunufaike na usafiri huu’’alisema mkazi huyo wa kitunda’’.






No comments:

Post a Comment