Thursday, October 25, 2012

BARABARA KUFUNGWA ZANZIBAR KUPISHA SHEREHE ZA EIDDI

Na Mwanshi wa Jeshi la Polisi Zanzibar
 ……………………….
Jeshi la Polisi zanzibar limetangaza kuzifunga baadhi ya barabara za mji wa Zanzibar ili kuwawezesha wananchi wakiwemo watoto wadogo kusherehekea siku kuu ya Eddi el Haji kwa usalama na amani.
 Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amezitaja baadhi ya barabara zitakazofungwa kwa muda wa siku nne kuanzia Ijumaa wiki hii hadi Jumatatu wiki ijayo kuwa ni ile inayotoka Mnazi Mmoja hadi Viwanja vya michezo vya Maisala, barabara ya kutoka Ofisi ya Baraza la Wawakilishi la Zamani kuelekea Viwanja vya Maisala na Barabara ya ya kutoka Ukumbi wa CCM kuelekea Mnazi Mmoja.
 Inspekta Mhina, amesema kuwa barabara hizo zitafungwa kuanzia majira ya saa 9.00 arasili hadi saa 4.30 usiku kwa kila siku muda ambao watu wengi watakuwa wamesharejea majumbani kwao baada ya kusherehekea siku hiyo.
 Awali akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mjini Zanzibar, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Ungauja ACP Aziz Juma Mohammed, alisema kuwa sherehe hizo zitaadhimishwa kwa muda wa siku nne mfululizo zitaanza Ijumaa ya Oktoba 26 hadi Jumatatu ya Oktoba 29 2012.

No comments:

Post a Comment