Wednesday, October 17, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE AANZA ZIARA YA SIKU NNE YA KITAIFA KATIKA NCHI YA FALME YA OMAN


 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi mwenyeji wake Sultani wa Oman Qaboos bin Said Al Said katika kasri ya AL Alam jijini Muscat Oman jana jioni muda mfupi kabla ya dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa kwa heshima yake.
 Sultani wa Oman,Qaboos bin Said Al Said akimtunuku Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete nishani ya juu ya heshima, Taifa la Oman wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake jana jioni katika kasri ya  AL Alam jijini Muscat Oman.
Sultan Qaboos bin Said Al Said akimpongeza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kumtunuku nishani ya juu ya heshima ya Taifa la Oman jana jioni katika kasri ya AL Alam. Jijini Muscat Oman jana jioni .Rais Kikwete aliwasili nchini Oman jana jioni kwa ziara rasmi ya siku nne. Picha na Freddy Maro
Juu: Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mwenyeji wake Sultani wa Oman Qaboos bin Said Al Said katika kasri ya Sultani jijini Muscat. Chini  Watoto  wakitanzania ambao wazazi wao wanaishi na kufanya kazi katika ubalozi wa Tanzania nchini Oman wakimkaribisha kwa maua Rais Dkt.Jakaya Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa  Muscat jana jioni.
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Sultani wa Oman Qaboos bin Said Al Said wakipokea heshima za viongozi muda muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuwasili jijini Muscat Oman leo mchana kwa ziara rasmi (State Visit) ya siku tatu nchini Oman.


Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mwenyeji wake Sultani wa Oman Qaboos bin Said Al Said katika kasri la Sultani jijini Muscat leo. Picha na Freddy Maro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anaanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku nne katika Taifa la Kifalme la Oman, ikiwa ni ziara ya kwanza ya Kiserikali kufanywa na Rais wa Tanzania katika nchi hiyo.

Rais Kikwete na ujumbe wake ameondoka mjini Dar es Salaam asubuhi ya leo, Jumatatu, Oktoba 15, 2012, kwenda Oman kuanza ziara hiyo inayofanyika kwa mwaliko wa Kiongozi wa Ufalme wa Oman, Mfalme Qaboos bin Said, ambaye atakuwa mwenyeji wake kwa siku zote nne.


Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Muscat, Rais Kikwete anatarajiwa kulakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Mheshimiwa Yousef bin Abdullah bin Alawi ambaye ataandamana naye hadi Jumba la Muscat Gate ambako Rais atapokelewa na Mfalme Qaboos. Kutoka hapo wataandamana hadi Kasri ya Kifalme ya Al Alam ambako atapokelewa rasmi kwa heshima zote za Kiserikali.


Shughuli kubwa ya jioni ya leo ya Mheshimiwa Rais itakuwa ni kufanya mazungumzo rasmi ya Kiserikali kati ya Serikali za Tanzania na Ufalme wa Oman na pia kuhudhuria dhifa rasmi ambayo Mfalme Qaboos atamwandalia mgeni wake kwenye Kasri ya Al Alam.


Kesho, Jumanne, Oktoba 16, 2012, Rais Kikwete atatembelea Jumba la Makumbusho la Majeshi ya Ulinzi ya Oman, atafungua Mkutano wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Oman, atashuhudia utiaji saini makubaliano ya mikataba miwili kati ya nchi hizo mbili, ukiwamo ule wa kuundwa kwa Baraza la Biashara la Tanzania na Oman na ule wa Kuendeleza na Kulinda Uwekezaji katika nchi hizo mbili.


Jioni, Rais Kikwete atatunukiwa nishani ya juu kabisa ambayo Ufalme wa Oman hutoa kwa viongozi wa nchi za nje ya First Order Medal kwenye Chakula Maalum cha Usiku kitakachoandaliwa na Mfalme Qaboos kwa heshima ya Rais Kikwete.


Rais Kikwete na ujumbe wake pia utakutana na kuzungumza na Watanzania wanaoishi Oman katika mkutano utakaofanyika kwenye Hoteli ya Kifalme ya Al Bustan.



No comments:

Post a Comment