Wednesday, October 17, 2012

HISTORIA YA JWTZ

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.

ASKARI WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA WAKIWA WAMETULIA WAKITAFAKARI JUU YA UL;INZI WA NCHI YETU

Kikundi cha Askari wa Jeshi la Nchi Kavu na Jeshi la Kujenga Taifa kikiwa kimesimama kwa ukakamavu siku ya Mashujaa.

Nchi yetu kama zilivyo baadhi ya nchi za Ki-Afrika kabla ya mwaka 1884 ilikuwa haina jina kamili ambalo lilijulikana, mpaka mipaka halisi ilipowekwa ya kugawa nchi za bara la Afrika na nchi yetu kuitwa Tanganyika iliyo jumuisha Rwanda na Burundi chini ya Utawala wa Kijerumani (German Osta Africa).

WAJERUMANI

Wajerumani waliitawala Tanganyika kuanzia mwaka 1884 – 1918.
Walianzisha jeshi lao lililojulikana kama SCHUTZTRUPPE ambalo lilikuwa na askari wapatao 3000, wengi wao walikuwa Wanubi toka Sudani.
Jeshi liliongozwa na Maafisa na askari wa Kijerumani wapatao 80.
Vita kuu ya kwanza ya dunia ilipoanza 1914 – 1918, Jeshi hilo lilipanuka na kufikia askari 12,000. 
Vita kuu ya kwanza ya Dunia ilipiganwa kuanzia mwaka 1914-18. Sehemu kubwa ya mapigano ilikuwa Afrika hasa Afrika ya Mashariki nchini Tanganyika amabalo lilikuwa ni koloni la Wajerumani waliokuwa wakipigana na Waingereza waliokuwa na Makoloni ya Kenya na Uganda wakisaidiwa na Wabeligiji toka Congo (DRC).

Viongozi wa Majeshi ya Wajerumani na Waingereza walikuwa ni Gen Paul-Emil Von Lettow Vorbeck aliyezaliwa mwaka 1874 (Mjerumani) na Gen Jan Christan Sumut ambaye alizaliwa mwaka 1870.

WAINGEREZA

Baraza la udhamini la Umoja wa Mataifa (The league of Nations) liliiweka Tanganyika chini ya udhamini wa Waingereza baada ya Ujerumani kushindwa Vita Kuu ya Pili. Waingereza waliunda Jeshi lao lililoitwa Kings African Rifles.
Kings African Rifles iliundwa na vikosi vya askari wa miguu, wahandisi wa medani, mawasiliano, mizinga na vikosi vya huduma. Vikosi vya Kings African Rifles vilikuwa Kenya 3rd & 5th Bn Tanganyika 1st 2nd &6th na Uganda 4th Bn.

UHURU WA TANGANYIKA

Tanganyika ilipata Uhuru tarehe 09 Desemba 1961 na siku hiyo Kings African Rifles (KAR) ilibadilishwa na kuwa Tangayika Rifles (TR). Pamoja na kubadilika jina Tanganyika Rifles ilikuwa na muundo sawa na Kings African Rifles (KAR).

MAPINDUZI YA ZANZIBAR

Mapinduzi ya Zanzibar yalifanyika tarehe 12 Januari 1964 kupinga utawala wa Kisultani.
Jeshi la Ukombozi wa Zanzibar Peoples Liberation Army PLA liliundwa baada ya Mapinduzi.

MAASI YA TANGANYIKA RIFLES
Jeshi la Tanganyika Rifles liliasi tarehe 20 Januari 1964 na maasi hayo kuzimwa 25 Januari 1964. Maasi yalihusisha vikosi vya DSM na Tabora 1st Bn na 2nd Bn.

MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR

Kuungana kwa Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Apr 1964 pia vijana waliobaki baada ya maasi toka Tanganyika Rifles waliungana na vijana jeshi la Ukombozi wa Wananchi wa Zanzibar (PLA) Peoples Liberation Army).


JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania lilianzishwa tarehe 01 Septemba 1964 baada ya Jeshi la Tanganyika Rifles lililoasi kuvunjwa.

MAFANIKIO YA JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

Kusaidia nchi za kiafrika ambazo zilikuwa bado hazijapata Uhuru kuanzia 1963 – 1994.

Mafanikio katika Operation mbalimbali:-

-Kushiriki katika utoaji huduma wakati wa maafa ya Kitaifa.
-Kushirikishwa katika ujenzi wa Taifa (Jeshi la Kujenga Taifa) na Jeshi la Kujenga uchumi (Zanzibar).
-Ulinzi wa amani.

Mafanikio ya Ushindi wa Vita vya Kagera (Operation Chakaza) iliyoanza tarehe 25 Oct 78 na kumalizika 25 Jul 79.

-Kulinda Uhuru na heshima ya nchi yetu baada ya kumfukuza Mvamizi.
-Makamanda na Wapiganaji kuelewa wajibu wao kwa Taifa.
-Mshikamano kitaifa kuanzia ngazi zote. 


No comments:

Post a Comment