Tuesday, October 23, 2012

WATEJA WA BARCLAYS BANK KUSHUHUDIA LIGI KUU YA ENGLAND (BPL) LIVE


 Mkuu wa Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania, Tunu Towo Kavishe (kushoto) akionyesha jezi halisi ya timu ya Arsenal, ikiwa ni moja ya zawadi watakazopewa washindi wa promosheni ya Ligi Kuu ya England (BPL) inayoendeshwa na benki hiyo. Mshindi mmoja katika kila droo hujishindia tiketi ya yeye na mwenzake kwenda kushuhudia moja ya mechi za ligi hiyo nchini Uingereza. Droo hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo mchana. Kulia ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Maggid Bakari na Mkuu wa Bidhaa, Huduma na Utafiti wa
benki hiyo, Samwel Mkuyu.
 England (BPL) inayoendeshwa na benki hiyo.
 Mkuu wa Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania, Tunu Towo Kavishe (kushoto) akionyesha jezi halisi ya timu ya Manchester ikiwa ni moja ya zawadi watakazopewa washindi wa promosheni ya Ligi Kuu ya
Mkazi wa Jiji la Dar es Salaam, Rukia Kizwi (kushoto) akitoa tiketi ili kumpata mmoja wa washindi wa promosheni ya Ligi Kuu ya England (BPL) inayoendeshwa na benki hiyo, wakati wa droo hiyo iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam. Mshindi mmoja katika kila droo hujishindia tiketi ya yeye na mwenzake kwenda kushuhudia moja ya mechi ya ligi hiyo nchini Uingereza na wengine wawili hujishindia zawadi ndogondogo. Droo hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano wa Barclays, Tunu Towo Kavishe, Mkuu wa Bidhaa, Huduma na Utafiti wa benki hiyo, Samwel Mkuyu, Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Bakari Maggid na Ofisa Mawasiliano wa Barlclays, Lilian Machare.

No comments:

Post a Comment