Sunday, October 21, 2012

MUSOMA UTALII YAJENGA CHUO CHAKE TABORA


Shabani Mrutu mkurugenzi wa Chuo Cha Musoma Utalii Tabora
  NA MWANDISHI WETU TABORA

UKOMBOZI wa taifa letu kwa kizazi cha sasa na kijacho,  jambo la
msimngi zaidi ni elimu bora ni suala muhimu sana ambalo litasaidia
kuondokana na hali ya umasikini,maradhi na ujinga ambao umekithiri
miongozi mwa watanzania waliowengi kwa sasa.

Chuo cha musoma utalii,kilichopo mkoani Tabora, ni chuo

kilichosajiliwa na “NACTE” kinachoendesha mafunzo ya kozi mbalimbali
na kimekuwa kikitoa elimu inayolingana na hali halisi ya sasa ya
sayansi na teknolojia.

Aidha chuo hicho kimekuwa kikitoa mafunzo ua juu ya kozi kama vile

uongozaji wa  watalii,hotel management,uwalimu wa chekechea,
uandishi wa habari na utangazaji, secretarial na Computer hali
iliyopelekea kufanikiwa  kutoa wahitimu bora waliofanikiwa kuajiriwa
na kujiairi ili kwenda sanjari na changamoto za soko la ajira ndani na
nje ya nchi.

Mkurugenzi wa chuo cha Musoma Utalii tawi la Tabora, Shabani

Mrutu,alisema hayo wakati alipokuwa akifanya mahojiano maalumu na
gazeti hili ofisini kwake alisema chuo kimekuwa ni chuo cha  mfano wa
kuigwa,na kimbilio la wengi na hadi sasa chuo hicho kimeanza ujenzi
wake.

Alisema ujenzi huo umekamilika kwa asilimia 80, ambapo kutakuwa na

mabweni yanayoweza kuchukua wanafunzi zaidi 200,vyumba vya madarasa
10,jengo la utawala la ghorofa na maktaba ya  kisasa,jiko la
kisasa,ukumbi na sehemu za  mapumziko.

Alisema kuwa mkoa wa Tabora una vivutio vingi vya kitalii lakini

haviendelezwi ipasavyo hivyo ujenzi wa chuo mkoani hapa ni ukombozi
mzuri ambao utasaidia vivutio hivyo kuonekana na hatimaye kukuza secta
ya utalii mkoani Tabora.

Mrutu alifafanua zaidi kuwa chuo hicho kilianzishwa mwaka 2004 kikiwa

na wanafunzi 42 na sasa kuna wanafunzi 280,ambapo chuo kilikua chini
ya usimamizi VETA.

Aidha mkurugenzi huyo aliongeza kuwa chuo hadi sasa,kimesajiliwa na

kutambulika na NACTE kwa barua ya awali yenye kumb. Namba
NACTE/BA/77/465/605/Vol 1/9 usajili ambao ulianza mwaka 2012.

Anabainisha kuwa chuo kina matawi mengi nchini ili kuwafikia vijana

wengi zaidi kwa gharama nafuu sana.

Mafanikio toka 2004 hadi sasa kampasi ya Tabora.


Mrutu anabainisha kuwa mafanikio kwa tawi la Tabora,ni kuongezeka kwa

wanafunzi toka 2004 wanafunzi 42 hadi 280 mwaka 2012.

Akizungumzia mafanikio katika utoaji wa elimu katika chuo  hicho,

mkuu huyo wa chuo alisema wamejipanga vyema kutoa elimu bora na zaidi
chuo kina kwa kuenmdelea kuongeza walimu ambapo hadi sasa kuna waalimu
18 wenye sifa zinazotambulika kisheria.

Alisema ili kuweza kutoa elimu bora pia wanafunzi wa chuo hicho

wamekuwa wakienda mafunzo ya vitendo kulingana na kozi wanazosoma
katika mikoa mbalimbali.

Mkurugenzi huyo anaongeza kuwa wanafunzi hupelekwa katika hotel kubwa

za kitalii,kampuni za uongozaji watalii ,TANAPA na kozi za ufundishaji
chekechea hupelekwa katika shule za kiingereza,wengine vituo vya radio
kwa wanafunzi wanaochukua masomo ya uandishi wa habari.

Alisema maeneo mengine ya kitalii wanafunzi hao hupelekwa kwenye

makumbusho ya Kwihara nje kidogo ya mji wa Tabora, sehemu ambayo
makumbusho hayo yana historia ya kipekee kwa mkoa na taifa kwa ujumla.

Akizungumzia muitikio wa wanafunzi  kujiunga na chuo ni mzuri kwani

kila wanapochukua wanafunzi kila muhula idadi huwa inaongezeka
kulingana mahitaji halisi,ambapo sifa zilizowekwa ni wanafunzi
waliohitimu kidato cha nne hadi cha sita.

Malengo na matarajio ya chuo.


Mkurugenzi huyo Shabani Mrutu, alisema chuo hadi sasa kinakamilisha

majengo yake tawi la Tabora,ambayo yanatarajiwa kukamilika ndani ya
miezi Tisa ujenzi huo unatarajia kukamilika kwa gharama ya zaidi ya sh
milioni 800.

Alisema malengo mengine ni kusajili  kozi nyingi zaidi kwenda

NECTA,sanjari na kusajili chuo kiweze kutoa elimu ya juu kutokana na
kozi zilizopo.

Aidha malengo mengine ni kuweza kusajili wanafunzi watakaofikia

1000,kuongeza matawi nchini ili chuo kiweze kutoa huduma bora zaidi
kwa jamii tena kwa gharama nafuu na kutoa elimu bora yenye ushindani
katika soko la ajira.

Kuhusu changamoto zilizopo.


Kuhusu changamoto zilizopo mkurugenzi huyo alisema chuo kimekuwa

kikikabiliwa na changamoto kadhaa ambazo ni uelewa wa jamii katika
vyuo binafsi kwani imejengeka fikra potofu vyuo binafsi wahitimu huwa
hawawezi kupata ajira na kwamba fikra hizo ni potofu kwani vyuo
binafsi na vya serikali vina nafasi sawa ilimradi viwe na usajili
unaotambulika serikalini.

“Ipo dhana ya namna hiyo lakini tumekuwa tukijitahidi sana kutoa elimu

kwa wazazi na zaidi ufaulu na ksaidia wanafunzi kujiajiri na kuajiriwa
kumekuwa kukitusaidia kuondoa dhana hiyo potofu.” Alisema.

Alitaja changamoto nyingine kuwa uelewa mdogo wa wazazi juu ya kozi ya

“Hotel Management,” kuwa ni kozi ya kihuni kiasi cha kuleta wanafunzi
kiduchu,ili hali si kweli ni kozi nzuri na ina uwanja mpana wa ajira
na uhuni ni tabia ya mtu binafsi.

Aliongeza changamoto nyingine ni hali ya kipato cha wazazi na walezi

na jamii kwa ujumla kwani imekuwa moja ya changamoto ya chuo kushindwa
kufikia malengo yake hasa kutokana na ulipaji mgumu wa ada kwa
wanafunzi,kwani “Wakazi wa mkoa wa Tabora wengi wao ni wakulima kwa
asilimia kubwa hivyo wengi husubiri kipindi cha msimu kimalipo ama
mvua inaponyesha vyema.”alisema.

Alisema hali hiyo hupelekea chuo kutofikia malengo yake ya kujiendesha

hasa ukizingatia chuo hakina ufadhili wowote zaidi ya kujiendesha
chenyewe.

Alisema chuo pia kinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vifaa na

hasa vinapopatikana huwa ni vya bei ya juu,huku  vifaa vya kozi za
utalii navyo huwa ni tatizo kubwa kupatikana.

Mkurugenzi huyo alitoa wito na ushauri kwa jamii kuendelea kukiamini

chuo cha Musoma Utalii,kwani toka kimeanzishwa kimeweza kutoa wahitimu
bora kwa asilimia 90 wamefanikiwa kujiajiri na kuajiriwa kote nchini.

“Tunaomba wazazi na jamii kwa ujumla kuendelea kuleta wanafunzi ili

waweze kupata elimu bora yenye kutambulika kitaifa na kimataifa.”
Aliongeza.

Aidha aliomba pia wazazi kuendelea kuchangia fedha za kwenda mafunzo

ya vitendo ,(Study Tour), kwani chuo kina ratiba ya kutembelea Mbuga
za wanyama mara tatu (3) kila mwaka ikiwa ni sehemu mojawapo ya
kuhamasisha utalii wa ndani kwa Watanzania kwa ujumla.

Alisema ana imani endapo chuo kitakamilika ujenzi wa majengo ya yake

ana imani mkoa wa Tabora ambao ni mkoa wenye historia ya
kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni utapiga hatua ya kimaendeleo na kutoa
ajira zaidi.

Mrutu anaongeza kuwa ni dhahiri mkoa wa Tabora una fursa nyingi sana

lakini bado hakuna jitihada za makusudi na hasa elimu kwa vijina wetu
kusoma ili kukabiliana na ushindani wa shirikisho la afrika mashariki
kwa sasa.

Hata hivyo mkurugenzi huyo amesifu kasi mkuu wa mkoa wa Tabora,Fatma

Mwassa katika usimaizi na kutoa vipaumbele ya elimu mkoani hapa kwani
dalili za mbadiliko ya elimu zimeanza kutoa picha ya mafanikio mazuri
tuendako.

Mrutu anaongeza kuwa mkuu wa mkoa wa Tabora,Fatma Mwassa amekuwa

mstari wa mbele zaidi katika kusukuma gurudumu la elimu kwa kuweka
mikakati madhubuti ya watoto hasa wa masikini waweze pata elimu
itakayosaidia kuondokana na umasikini.

Mkurugenzi huyo anasema kwa sasa chuo cha Musoma Utalii ni kimbilio la

wanyonge kwani kimaonekana ni mkombozi zaidi.

No comments:

Post a Comment