Sunday, October 21, 2012

HUDUMA YA ELIMU MTANDAO KUPITIA MAKTBA YAWAFIKIA WANAFUNZI WA CHANGO'MBE MSINGI

 Meneja Mradi wa shirika lisilo la kiserikali kutoka Ujerumani ( EIFL) Monica ELBERT, akiwaangalia baadhi ya wanafunzi  wa shule ya msingi Chang’ombe  Mazoezi  wilaya  ya Temeke jijini Dar- es- Salaam, wakati   wakifanya  mafunzo  ya pamoja  jinsi  ya  kutumia  teknolojia   ya upashanaji wa habari na mawasiilano  kupitia mtandao.  

Mradi huo wa mafunzo  ujulikanao  (Public Library Innovation Programme- PIP- )  Kwa kupitia mradi huo wanafunzi  wataweza  kupata taarifa  mbalimbali  kirahisi kwaajili  ya masomo yao na taarifa mbalimbali za kila siku, Meneja  wa mradi huo  amefurafahishwa sana baada ya kuhojiana na wanafunzi hao na kumueleza kwamba ni ukombozi kwao kwani  baada ya kumaliza mafunzo, elimu  itakuwa imewasaidia sana kuwarahisishia masuala mbalimbali ya masomo pamoja kupata taarifa mbalimbali
 Baaadhi ya wanafunzi wakifanya mazoezi.
Baaadhi ya wanafunzi wakifanya mazoezi. Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO

No comments:

Post a Comment