Thursday, October 18, 2012

WATAKA MIKATABA IANDIKWE KISWAHILI




Na Lucas Raphael ,Sikonge  



BAADHI ya wananchi wa kata ya kipili wilayani sikonge mkoani Tabora jana walisema kuwa mikataba itakayo sainiwa na serikali isainiwe bungeni pamoja na kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili.

Wakizungumuza kwa nyakati mbalimbali wakati wakitoa maoni ya katiba mpya wananchi wa kata hiyo walisema kuwa baadhi ya viongozi wanaingia mikataba ambayo haina manufaa kwa Taifa badala yake mikataba hiyo huwanufaisha baadhi ya viongozi.

Walisema kuwa katiba itakayo undwa iweke sheria madhubuti ya kuhakikisha mikataba yote inafungiwa mbele ya bunge pamoja na kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili ili kila mwananchi aweze kuielewa.

Waliongeza kuwa mikataba hiyo isiwe siri kama baadhi ya mikataba hapa nchini ambapo haifahamiki kwa wananchi bali mikataba hiyo ifahamike ili kila Mtanzania aelewe mkataba huo unavyo kwenda.

Wakiendelea kutoa maoni hayo waliomba katiba itakayo undwa iweke uwazi wa mikataba hiyo pamoja na kuzingatia maoni hayo yaliyotolewa na wananchi hao.

‘’Tunataka katiba hii iweke mkazo juu ya hili kwani tunapata adha sana sheria ndogo ndogo ziwabane wawekezaji hawa’’ alisema mkazi mmoja wa kijiji hicho. 

Waliongeza kuwa richa ya mikataba hiyo kuhakikiwa na bunge mkataba huo uwanufaishe wananchi waeneo husika kwa kodi za mradi huo pamoja na huduma za kijamii ili wananchi waweze kunufaika na mikataba itakayo endelea kuwekwa na serikali ikiwa ndani ya katiba mpya.


‘’Tuna taka mikataba yote tuifahamu,iandikwe kwa lugha nyepesi pia i sambazwe kwa wananchi ili kila mwananchi afahamu mikataba hiyo tofauti na sasa baadhi ya mikataba imeandikwa kiingereza pia haionekani ni siri kubwa kwa watu’’alisema Edward Nalali.

Mbali na maoni hayo wakiendelea kuchangia walisema kuwa kuwepo na tume huru ya uchaguzi ambayo itakayo jitegemea yenyewe pamoja na serikali iwajali wajane,Virema,wazee pamoja huduma za Afya.

Tume huru ya kukusanya maoni ya katiba mpya kundi la mkoa wa Tabora linaendelea wilayani sikonge baada ya kuhitimisha zoezi hilo wilayani urambo huku likiongozwa na mwenyekiti wake Fatuma said Ally.

Mwisho.


No comments:

Post a Comment