Sunday, October 28, 2012

SIMBA YAITUNGUA AZAM FC YA CHAMAZI MAGOLI 3-1 UWANJA WA TAIFA


Beki wa timu ya Simba Shomari Kapombe akimiliki mpira mbele ya Ibrahim Shikanda mshabuliaji wa timu ya Azam FC katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii jijini Dar es salaam, mpira umekwisha  Simba imeibuka  kwa ushindi mnono wa magoli 3-1 dhidi ya Azam FC ambayo yamefungwa na Felix Sunzu kwa kichwa na Emmanuel Okwi la pili na la tatu lililofungwa kipindi cha pili dakika za mwanzomwanzo, goli la Azam limefungwa na mshambuliaji John Boko.
Huko Arusha timu ya Yanga ilikuwa mgeni wa timu ya JKT Oljoro ya huko katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, ambapo Yanga imeibuka na ushindi wa goli moja lililofungwa na Mchezaji Mbuyu Twite
Wachezaji wa Simba wakishangilia mara baada ya kupata goli la pili katika mchezo huo.
Wachezaji wa timu aAzam FC wakisalimiana na wachezaji wa timu ya Simba kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Mashabiki wa timu ya Azam wakiishangilia timu yao wakati ikicheza na timu ya Simba uwanja wa Taifa jioni hii.Picha/Habari Na Full Shangwe Blog

No comments:

Post a Comment