Tuesday, October 23, 2012

SPIKA ANNA MAKINDA AKISHIRIKI MKUTANO WA 127 WA IPU ,MJINI QUEBEC,CANADA AKUTANA SPIKA WA MOROCCO

 

 

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na mratibu wa mahusiano baina  ya Global Fund na Mabunge Duniani Ndg. Svend Robinson, walipokutana  kabla ya kuanza kwa mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU)  unaofanyika Mjini Quebec, Canada.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimtambulisha Mbunge wa Bunge la Afrika  Mashariki kutoka Tanzania Mhe. Dr. Perpetua Nderakindo Kessy kwa Balozi wa Tanzania Chini Canada Mhe. Alex Massinda kabla ya kuanza kwa mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika Mjini Quebec,  Canada.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akifuatilia taarifa mbalimbali na maazimio  ya Mkutano wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) wakati wa ufunguzi wa  Mkutano wa 127 wa IPU Mjin Quebec, Canada. Kushoto kwake ni Balozi wa  Tanzania Chini Canada Mhe. Alex Massinda na Mhe. Hamad Rashid Mohamed.
Mkurugenzi wa Maktaba na Utafiti wa Bunge Ndg. Kileo Nyambele anaye muwakilisha  katibu wa Bunge Dkt. Thomas kashilila akishiliki kikao cha makatibu wa  Mabunge yote wanachama wa Mabunge ya Dunia (IPU) katika Mkutano wa 127  wa chama hicho mjini Quebec, Canada. Kulia kwake ni Afisa dawati la IPU  kutoka Tanzania Ndg. James Warbarg.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiongoza ujumbe wa Tanzania kupiga kura  kuingiza agenda mojawapo kati ya agenda 5 za dharura zilizowasilishwa   kwa udharura katika mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU)  ili zijadiliwe pia. Tanzania iliungana na nchi za Afrika kupigia kura  agenda ya kujadili hali ya usalama katika nchi ya Mali pamoja na agenda  iliyowasilishwa na Uingereza kujadili kwa udharura swala la hatma ya  Usalama na Misaada wa Kibinadamu Nchini Syria na nchi Jirani. Kushoto  kwake ni Balozi wa Tanzania Chini Canada Mhe. Alex C. Massinda na Mhe.  Hamad Rashid Mohamed.
Spika wa Bunge akitoka katika ukumbi wa Mikutano mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kwanza katika Mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) mjini Quebec, Canada. Kushoto kwake ni Mhe. David Kafulila  anayehudhuria Mkutano huo pia.
Mhe. Anne Makinda akitoka katika Mkutano na Spika wa Bunge la Morocco Mhe. Karim Ghellab kwa lengo la kufanya nae mazungumzo ya faragha kuimarisha uhusiano baina ya mabunge ya Tanzania na Morroco.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisisitiza jambo wakati alipokutana na  Spika wa Bunge la Morocco Mhe Karim Ghellab kujadili namna bora ya  kuimarisha mahusiano baina ya mabunge ya nchi zao. Tanzania ilipeleka  ujumbe wa Wabunge kutoka kamati ya Mambo ya Nje, ulinzi na Usalama  kutembelea Bunge la Morocco Aprili mwaka huu ikiwa ni sehemu ya  kuimarisha mahusiano baina ya nchi hizi mbili.
Spika wa Bunge la Morocco Mhe Karim Ghellab akimkabidhi Mhe. Spika zawadi mara baada ya kufanya nae Mazungumzo.
Ujumbe kutoka Bunge la Tanzania katika Mkutano wa 127 wa IPU Mhe. Hamad Rashidna Mhe. Suzan Lyimo wakifuatilia kwa makini mada kuhusu  “Multilateralism and the role of parliament in parliamentary diplomacy”  wakati wa mkutano huo Mjini Quebec, Canada.

No comments:

Post a Comment