Wednesday, October 17, 2012

ASKARI WATAKA USAWA JESHINI.





Na Lucas Raphael,Urambo 

Askari polisi na Magereza wilayani urambo mkoani Tabora wamesema kuwa majeshi yote nchini yawe na usawa katika utendaji pamoja na uwajibikaji wa wakazi zao.

Wakitoa maoni ya katiba mpya mbele ya tume ya maoni ya kukusanya maoni kundi la Tabora walisema kuwa Askari polisi na Askari Magereza wapewe haki zinazo fanana na Askari wa jeshi la wananchi(JWTZ).

Akizungumuza katika kikao hicho cha kutoa maoni Osca mwenye namba E 7276 askari magereza alisema kuwa usawa huo ni kutokana na kipato cha Askari wa Jeshi la wananchi (JWTZ) nikikubwa tofauti na Askari wengine wa majeshi mengine ikiwa na Jeshi la Polisi pamoja na Jeshi la Magereza.

Aliongeza kuwa Askari hao wanafanya kazi kwa pamoja na kutumikia Taifa hili pamoja hivyo usawa katika utendaji kazi utekelezwe.

Osca akitoa maoni yake alisema kuwa Majeshi yote yalipwe stahiki sawa kutokana na kiapo chao kuapa kulitumikia taifa hili kwa pamoja.

’’Tulipwe kwa sawa nasisi tunafanya kazi kama hizo kama ikitokea vita tutaenda wote hivyo ni bora tukawa tunalipwa posho sote ili kutoa utabaka katika majeshi hivyo katiba hii izingatie hilo’’alisema Askari huyo .

Wakizungumuza kwa nyakati mbalimbali Askari hao walisema kuwa upandishwaji wa vyeo haufuati taratibu za kisheria kutokana na upendeleo kwa baadhi ya viongozi wa ngazi za juu.

Wakitoa maoni yao walisema kuwa vyeo hivyo vipandishwe kila baada ya miaka mitatu kama ilivyo kuwa hapo awari ili kila Askira aweze kupandishwa vyeo vyao na kuongeza kuwa sheria zilizopo katika majeshi zifuatwe na utekelezaji wake utekelezwe kiusawa.

Joakimu Nindi Mratibu wa Jeshi la Magereza wilayani Urambo akitoa maoni yake alisema kuwa majeshi yote yasifungamane na siasa ili kila jeshi lifanye kazi yake kwa uhuru zaidi.

Tume hiyo kundi la tabora limehitimisha zoezi hilo wilayani Urambo ambapo likitarajia kuelekea wilayani sikonge kuendelea na mchakato huo wa kukusanya maoni hayo.

MWISHO.


No comments:

Post a Comment