Thursday, October 18, 2012

POLISI WALALAMIKIWA KWA VITENDO VYA KIKATILI




 Na Lucas Raphael,Tabora

BAADHI ya wananchi wilayani Nzega Mkoani Tabora wamewalalamikia baadhi ya Askari polis wilayani hapa kwa kutumia nafasi  zao kuwa tendea kinyume na maadili ya kazi hiyo.

Wakizungumza na ukurasa huu kwanyakati tofauti wilayani hapa wamesema kuwa baadhi ya Askari hao hutumia nafasi zao kwa kuwa nyanyasa wananchi ikiwa na kuwa bambikizia  makosa mbalimbali ambayo yapo kinyume na sheria za hapa nchini.

Mkazi mmoja wa nzega mjini akizungumuzia mikasa ya Askari hao kuwa baadhi yao hufanya makosa lakini raia akifanya kosa kama alilofanya Askari huyo huchukuliwa sheria ikiwa na kubambikiziwa kesi mbalimbali.

‘’mfano Askari anaendesha pikipiki bira kofia tena kalewa Askari huyo akimuona raia anaendesha pikipiki bila kofia anamchukulia hatua kari na kumbambikizia makosa je hapo ni haki? Nani awe mfano kwa mwenzie’’alisema mkazi huyo jina lake limehifadhiwa.

Wameeleza kuwa kitendo hicho kinawafanya wananchi hao kutokuwa na imani na baadhi ya Askari katika utendaji wao wa kazi.

Walisema kuwa baadhi ya Askari Polis wilayani hapa wanafanya kazi kwa kufuata maadili ya kazi hiyo hali ambayo mahusiano mema na wananchi wanapata hasa katika suala la polis jamii na kuongeza kuwa Askari wa polis jamii waweke mahusiano mema na wananchi ili kuweza kupata taarifa mbalimbali za wahalifu.

Waliziomba taasisi husika wilayani hapa kufuatilia suala hilo iliwananchi hao waendelee kuwa na imani na Askari hao pamoja na kutiisheria za nchi.

Kaim kamanda wa polisi mkoa ambaye ni mkuu wa upelelezi mkoa Edward Bukombe aliwataka wananchi kutoa taarifa kwa ofisi ya mkuu wa polis wilaya ili hatua kali zi chukuliwe dhidi ya Askari huyo.

‘’Askari Polis ni kioo cha jamii hivyo wanatakiwa kufuata maadili yao ili raia afurahi na huduma hiyo paolis anapaswa kutii sheria ili raia afuate polis wangu waache tabia hiyo vinginevyo sheria itachukua nafasi yake’’alisema Mkuu wa upelelezi huyo.

Bukombe alisema kuwa Askari polisi atakaye bainika anafanya kazi kinyume na maadili ya hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ikiwa na kufikishwa mahakamani.

Aliwataka Askari polisi mkoani hapa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya jeshi hilo pamoja na kuweka mahusiano bora na wananchi ili kudumisha polis jamii.

Mwisho.


No comments:

Post a Comment