Sunday, October 28, 2012

FM ACADEMIA,WAZEE WA NGWASUMA KUWASHA MOTO NDANI YA FRANKMAN HOTEL TABORA 1/11/2012





Mkurugenzi mtendaji Kitumbo Security,Yusuph Kitumbo
 Kampuni ya Ulinzi nchini Kitumbo Security Guard imeandaa burudani kabambe itakayoletwa kwenu na Bendi ya Muziki wa Dansi nchini FM ACADEMIA,WAZEE WA NGWASUMA  siku ya Alhamisi hii ya  tarehe 1/11/2012 katika ukumbi wa Frankmann Hotel mjini Tabora kuanzia majira ya saa moja usiku hadi majogoo. 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kitumbo Security,Yusuph Kitumbo, lengo la kuandaa burudani hiyo imetokana na kutekeleza maombi ya wakazi wa Tabora ya kutaka kuwaona FM ACADEMIA na vitu vyao adimu ambavyo mara nyingi wamekuwa wakiwashuhudia kwenye luninga pekee na sasa umefika wakati wa kuwaona LIVE bila CHENGA katika ukumbi huo wa Frankmann Hotel.

Kitumbo amesema FM ACADEMIA ni bendi maarufu nchini na kwasasa imekwisha jichukulia umaarufu mkubwa hapa Ulimwenguni na hivyo kuwataka wapenzi wa burudani mkoani hapa kuhudhuria katika burudani hiyo bila kukosa.

Aidha kuhusu kiingilio Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa ni kiasi cha shilingi 10,000/=  na huku akisisitiza kuwahi mapema kuingia ukumbini ili kuweza kujionea kila kitu kilichoandaliwa.

No comments:

Post a Comment