Tuesday, October 23, 2012

KATIBA IRUDISHE JESHI LA KUJENGA TAIFA JKT


WAKAZI WA  kata za kakola  na kalunde wilaya ya Tabora mjini mkoani hapa wamesema kuwa katiba itakayo patikana irejeshe jeshi la kujenga taifa kwa vijana wanaohitimu Elimu ya kidato cha sita ambao wanatarajia kuingia vyuo vikuu ili kuwajenge uzalendo kwa nchi yao. 

Wakizungumuza kwa nyakati mbalimbali wananchi hao mbele ya tume ya kukusanya maoni ya katiba walisema kuwa utaratibu huo ukirejeshwa utadumisha utamaduni na uzalendo wa mtanzania ambao unaelekea kupotea kwa wananchi.

Walisema katiba hiyo ikizingatia mambo hayo kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na elimu ya juu mpaka wapitie kozi hiyo fupi itaongeza maadili ya mtanzania ambayo yanazidi kutokomea kufuatia kuingiliwa na tamaduni za nchi za maghalibi.

Peter Manzilili mwalimu mkuu wa shule ya msingi umanda akitoa maoni yake ya kupata katiba mpya alisema kuwa Jeshi la kujenga Taifa likianzishwa litaongeza mapenzi kwa kizazi hiki ikiwa na kukabiliana na matatizo ya ajira kwa vijana ambapo imekuwa ni kelele kila kona.

Mafunzo hayo yakiendeshwa vizuri kwa kufuata utaratibu vijana wengi watapata fursa ya kujiajili kutokana namafunzo hayo ikiwa na kufanya kazi kwa bidii tofauti na wakati huu.

Alisema kuwa katiba hiyo ikizingatie hayo vijana watafanya kazi kwa bidii ikiwa na kuipenda kazi nchi yao tofauti na sasa vijana wengi hawana uzalendo. 

‘’endapo katiba hii ikaliweka suala hili naimani kabisa vijana watajiajili na wengine kupata kazi na kuipenda zaidi nchi yao kama vijana wa zamani ambao sasa ni babu zetu bado wanaipenda nchi hii kutokana na mfumo huo wa JKT’’alisema mwili huyo. 

Rusi Ismaili mkazi wa kata ya kakola aliongeza kuwa utaratibu huo ukirejeshwa hata wa naume watasitisha kuwa piga wake zao kutokana na mafunzo hayo kufundishwa kupendana na uzalendo kwa ujumla.

Aliongeza kuwa kwa mufumo huo unyanyasaji wa kijinsi utapungua kwa wanawake pamoja na haki zote za wananwake zitapatikana kupitia Jeshi hilo. 

’’kama kweli tunataka mabadilio basi katiba mpya irejeshe jeshi hili ili vijana wetu wajifunze maadili uzalendo hapo tutapata mabadiliko ya kutosha na Tanzania hii itakuwa safi’’alisema Rusi.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment