Thursday, October 25, 2012

MHE .HAMAD RASHI ATEULIWA KUWA MJUMBE WA KAMATI YA UKAGUZI WA HAESABU ZA NDANI IPU


Mhe. Hamad  Rashid Mohamed akifuatilia Mjadala wa  kamati ya Chama cha Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mjini Quebec, Canada, kuhusu maswala ya umoja wa mataifa. Mada kubwa ilikuwa kuangalia kama kweli Umoja wa Mataifa unalichukulia swala la demokrasia duniani kwa dhati.Picha  na Owen Mwandumbya
 ……………………………………………………….

Mbunge wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano wa Chama cha Mabunge Duniani Mhe. Hamad Rashid Mohamed ameteuliwa na kamati tendaji ya chama cha Mabunge duniani (IPU) kuwa mjumbe wa kamati ndogo ya ukaguzi wa ndani kwa mahesabu ya mwaka 2013 ya chama hicho.
Uteuzi huo ulifuatia pendekezo la umoja wa Mabunge ya Afrika lililowasilishwa na katibu mkuu wake Koffi N’Zi tarehe 22 Oktoba, 2012 kufuatia kikao cha wajumbe wa umoja wa Mabunge ya Afrika kumchagua Mhe. Hamad kuwakilisha Afrika kuwania pendekezo hilo mbele ya kamati tendaji ya chama hicho.
Mhe. Hamad Rashid Mohamed, hii ni mara ya pili kuiwakilisha Tanzania na Afrika katika kamati mbalimbali za IPU ambapo mwaka jana katika Mkutano uliofanyika Mjini, Benn, Uswis, alichaguliwa kuwa mjumbe wa Kamati ya Fedha na Uchumi ya IPU cheo ambacho anakitumikia hadi hivi sasa.
Katika kamati hiyo ya ukaguzi wa ndani, Mhe. Hamad Rashid atafanya kazi pamoja na mjumbe mwingine aliyeteuliwa Mhe. Duarte Pacheko kutoka Ureno, ambapo wanatarajia  kutoa taarifa ya kazi yao mwaka 2014 katika mkutano mkuu wa IPU.
Katika hatua nyingine, Wabunge vijana wametakiwa kuwa chachu ya maendelo katika nchi zao kwa kushawishi kutengeneza mazingira ya upatikanaji wa ajira kwa vijana katika kipindi hiki cha uchumi wa kitandawazi.
Hayo yamesemwa jana na Mtaalamu wa maswala ya ajira kutoka shirika la la kazi la umoja wa mataifa (ILO) alipo toa maada katika mjadala wa Wabunge Vijana kujadili na namna ya kupunguza ajira kwa vijana hususani katika kipindi hiki cha uchumi wa utandawazi.
Mtaalamu huyo amesema ni wajibu wa wabunge kuwa na ushawishi mkubwa kwa serikali zao na baadhi ya taaisisi zinazotoa ajira ili kuwa na sera madhubuti kwa ajira za vijana hususani wanaomaliza vyuo kwa lengo la kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.

No comments:

Post a Comment