Thursday, October 25, 2012

MIKIDADI MAHMOUD MWENYEKITI WA BODI MISS UTALII TANZANIA




Bodi ya Miss Tourism Tanzania Organisation,yenye dhima ya kikomo ya kuaandaa na kuendesha mashindano ya Miss Utalii Tanzania ,imemteua Ndugu Mikidadi Mahamoud kuwa mwenyeketi ya bodi ya Mashindano ya Miss Utalii Tanzania. Uteuzi huo utakuwa ni wa miaka mitatu kuanzia tarehe 1-10-2012.

Akuthibitisha uteuzi huo, Gideon Chipungahelo,Rais wa Miss Utalii Tanzania, hatua hii ni moja ya utekelezaji mpango mkakaeu wa miaka mitano wa kuimalisha mashindano na mfumo wa uongozi wa mashindano haya. Ambapo sasa tunakuwa na bodi ya mashindano na bodi ya taifa ya ushauri ambayo
itajumuisha wadau mbalimbali wa sekta ya utalii na serikali. Tayali tumeiandikia serikali kupitia Bodi ya Utalii Tanzania, tukiiomba kuwa na wajumbe katika bodi ya Taifa ya Miss Utalii Tanzania, ambapo kutakuwa na wajumbe pia kutika katika mamlaka mbalimbali za Utalii, Utamaduni, Mazingira, Elimu, Afya, Uwekezaji, Jinsia na asasi za kupambana na umasikini kupitia utalii na utamaduni. Mamlaka na Asasi hizo ni pamoja na Mamlaka za Hifadhi za Taifa, Bodi ya Utalii, Bodi ya Madini, Kurugenzi ya Utamaduni, Kurugenzi ya Utalii, Kituo cha uwekezaji Tanzania, Kurugenzi ya Mazingira na Tanzania Association for Tour operators.

Lengo la kufanyia mabadiliko ya mfumo wa uongozi na uendeshaji ni pamoja na kupanua wigo wa ushiriki wa mamlaka za umma na za binafsi katika uendeshaji wa mashindano haya,ambayo hakika ni alama ya urithi wa taifa na muhimu sana katika kuhamasisha ukuaji wa utalii wa Tanzania na kuhamasisha Utalii wa ndani,utalii wa kitamaduni,utumiaji wa bidhaa za kitanzania,utalii wa

michezo,utalii wa mikitano,pia kuhamasisha vita dhidi ya uharibifu wa mazingira,uwundaji haramu,uvuvi haramu,tamaduni kongwe na potofu,vita dhidi ya ujinga,umasikini na maradhi.

Bodi katika kumteua Ndugu Mikidadi Mahamoud kuwa mwenyekiti wa bodi,imezingatia busara,hekima na uzoefu wake mkubwa katika katika Nyanja za kitaifa na kimataifa za michezo,utangazaji, na uhamasishaji

No comments:

Post a Comment