Sunday, October 28, 2012

HEREHE ZA HARUSI SIKU HIZI MMMMH!!....BALAA TUPU

TUNAMWAGA RADHI;....Baadhi ya waalikwa katika moja ya sherehe ya harusi iliyokuwa ikifanyika kwenye ukumbi wa African House Tabora mjini wakiwa wanafanya vitu vyao,kibaya zaidi wengiwao ni wake za watu.

Vijembe na vikumbo vilitawala huku kila mmoja akijiachia anavyotaka yeye haijalishi kucheza na kupandisha nguo juu ili mradi nyeti zionekane hata mbele ya watoto wadogo.


Kulala chali au kulalia kifua na kuonesha mitindo mbalimbali ya tendo fulani ilikuwa ni kitu cha kawaida kabisa ingawa wengine walidiriki hata kuonesha namna walivyovipamba viuno vyao kwa shanga za aina na rangi mbalimbali hadharani.

BAADHI YA WATOTO TABORA HATARINI KWA PICHA ZA NGONO KWENYE MTANDAO


Hii sasa ina ashiria hatari kwa watoto kutumia muda mwingi katika kuperuzi picha za ngono kwenye mtandao.

Kwa mara ya kwanza nilipokuwa nikifika kwenye Internet Cafe ili niweze kuangalia mambo mbalimbali yaliyojiri ulimwenguni,nilikuwa nikishuhudia watoto nao wanaingia na kuomba muda wa kuperuzi kwenye mtandao kwa muhudumu kati ya dakika 30 hadi dakika 120.

Suala la kulipia muda huo kwa watoto niliobahatika kuwaona haikuwa shida sana,na kila ninapowakuta kwenye kompyuta wanakuwa bize sana hali iliyonilazimu nianze kuwafuatlia na kutaka kujua nini wanafanya kwenye mitandao hiyo.

Wapo niliowakuta wakiangalia picha za wachezaji wa mpira wa miguu na wasanii maarufu duniani,hilo halikunipa shida kama lile la baadhi yao tena waliowengi walikuwa wakitumia mitandao ya kijamii kama FACEBOOK. 

Nilipojaribu kumuuliza mmoja niliyekumbana nae,..hakuwa tayari kunijibu bali alikuwa kimya huku akizidi kuangalia kile kilichomleta hapo kwenye Internet Cafe.

Kwakuwa jicho halina mpaka,na kwa vile nimekaa kwenye kiti kilichopo jirani naye, nilijionea kitu ambacho sikufikilia kama mtoto mdogo kama yule angeweza kutafuta mambo makubwa kama hayo kupitia mtandao wa Google.

Ni picha za Ngono,tena chafu zisizosatahili hata kuangaliwa na mtu mzima tena mwenye akili timamu.

Pasipo shaka yoyote mtoto huyo aliendelea kujivinjali kwenye picha hizo zikiwemo za mnato na zile za video.

Jamani,jamani,jamani,......tena kibaya zaidi nikamsikia vizuri akimlalamikia yule mhudumu wa Cafe hiyo..."Dada mbona hii kompyuta haina sauti,...sasa mi ntaangaliaje video za bila sauti?''alikuwa akisema mtoto huyo wakati akiangalia kupitia Youtube huku akionesha kana kwamba ile ilikuwa haki yake ya kimsingi ambayo hajatekelezewa.

Hofu yangu watoto wetu wanaingia hatarini muda si mrefu kutokana na jambo hili.         

FM ACADEMIA,WAZEE WA NGWASUMA KUWASHA MOTO NDANI YA FRANKMAN HOTEL TABORA 1/11/2012





Mkurugenzi mtendaji Kitumbo Security,Yusuph Kitumbo
 Kampuni ya Ulinzi nchini Kitumbo Security Guard imeandaa burudani kabambe itakayoletwa kwenu na Bendi ya Muziki wa Dansi nchini FM ACADEMIA,WAZEE WA NGWASUMA  siku ya Alhamisi hii ya  tarehe 1/11/2012 katika ukumbi wa Frankmann Hotel mjini Tabora kuanzia majira ya saa moja usiku hadi majogoo. 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kitumbo Security,Yusuph Kitumbo, lengo la kuandaa burudani hiyo imetokana na kutekeleza maombi ya wakazi wa Tabora ya kutaka kuwaona FM ACADEMIA na vitu vyao adimu ambavyo mara nyingi wamekuwa wakiwashuhudia kwenye luninga pekee na sasa umefika wakati wa kuwaona LIVE bila CHENGA katika ukumbi huo wa Frankmann Hotel.

Kitumbo amesema FM ACADEMIA ni bendi maarufu nchini na kwasasa imekwisha jichukulia umaarufu mkubwa hapa Ulimwenguni na hivyo kuwataka wapenzi wa burudani mkoani hapa kuhudhuria katika burudani hiyo bila kukosa.

Aidha kuhusu kiingilio Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa ni kiasi cha shilingi 10,000/=  na huku akisisitiza kuwahi mapema kuingia ukumbini ili kuweza kujionea kila kitu kilichoandaliwa.

MABINGWA WA BALIMI BOAT RACE KAGERA WAPATIKANA



 Katibu Tawala wa Manispaa ya Bukoba Clement Ndiomukama, akimkabidhi kitita cha Tsh.900,000 Nahodha wa timu ya Kabanga Bushasha, Eliudi Prospa baada ya kuibuka mabingwa kwenye mashindano ya (Mitumbwi)  Balimi Boat Race Wilayani Bukoba Mkoani Kagera jana ambapo washiriki walishindana kuendesha  mitumbwi kwa makasia.
 Mabingwa wa mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) Mkoani Kagera  upande wa wanaume timu ya Kabanga Bushasha wanaume wakishangilia mara baada ya kuwa mabingwa wa mkoa huo na kukabidhiwa jumla ya shilingi laki tisa (900,000) kama zawadi ya ushindi wa kwanza.
 Mabingwa wa mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) Mkoa wa Kagera upande wa wanawake Timu ya Seleka kutoka Musila, wakishangilia mara baada ya kuwa mabingwa wa mkoa huo na kukabidhiwa jumla ya shilingi laki saba (700,000) kama zawadi ya ushindi wa kwanza.
 Katibu tawala wa Manispaa ya Bukoba Clement Ndiamukama, akifungua mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) yaliyofanyika Wilayani Bukoba Mkoani Kagera ambapo zaaidi ya timu 50 zenye watu watano kila timu zilishiriki, ambapo walishindana kupiga kasia kwa umbali wa Kilometa 3 kwenda na kurudi, kushoto ni Meneja wa Mauzo wa Kanda ya Ziwa Endrew Mbwambo na Afisa wa Sumatra Kapteni Alex Katama.
 Meneja wa Bia ya Balimi Edith Bebwa(kulia) akizungumza na washiriki wa mashindano ya Balimi Boat Race Wilayani Bukoba Mkoani Kagera mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo ambapo timu tano zitakwenda kuwakilisha mkoa huo kwenye fainali zitakazofanyika mkoani Mwanza Disemba mwaka huu.
 Waokoaji wakiwakoa wapiga kasia kinamama ambao walipinduka
Mabingwa Wanaumr Wakishangilia Baada Ya Kuwasili


WASHIRIKI wa shindano la mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race) ambayo ni maalum kwa mikoa ya kanda ya ziwa wametakiwa kutumia pesa wanazozipata kwaajili ya kujiendeleza kwenye miradi ya maendeleo.
 
Akizungumza mara baada ya mashindano hayo Meneja wa Kinywaji hicho Cha Balimi Edith Bebwa, alisema lengo la mashindano hayo ni kutoa shukrani na kuwawezesha wanywaji wake hivyo wanapaswa kuzitumia kwenye kujiendeleza kwenye miradi yao.
 
“Nawaomba mlioshinda na washiriki wengine ambao pia mmepata pesa hizo mzitumie kwenye miradi yenu kama ni mvuvi basi ongeza chombo kingine au nyavu ili mradi uzitumie kwenye uzalishaji” alisema Bebwa.
 
Awali akifungua mashindano hayo Katibu Tawala wa Manispaa ya Bukoba Clement Ndiamukama aliwataka washiriki watakaoshinda kutobweteka na ubingwa badalayake wajipange kwa mazoezi ili kwenye fainali ya mashindano hayo waupe heshima Mkoa wa Kagera.
 
“Tunataka mtuletee heshima kwahiyo wale watakaoshinda watambue wajibu huo wakuletea heshima Mkoa,” alisema Ndiomukama.
 
Mashindano hayo ambayo yalianza Mkoani Kigoma October 27 mwaka huu yanatarajiwa kumalizika kwenye fainali zitakazofanyika mwezi Disemba mwaka huu Mkoani Mwanza.

VOTES FOR KIMANJARO ,NGORONGORO AND SERENGETI ARE STILLNEEDED:

Votes for Kilimanjaro, Ngorongoro and Serengeti are still needed! Send a list of your top 7 wonders in Tanzania (the 3 above and any four from TANAPA) to vote@sevennaturalwonders.org, writing TANZANIA on the subject field! http://sevennaturalwonders.org/tanzania/

WAMBURA APANDA CHATI ECAPBA


 
BONIFACE WAMBURA
Boniface Eambura ambaye kwa sasa ndiye Menyekiti wa kamatiu ya Viwango ya Chama cha  Ngumi za Kulipwa la Afrika ya Mashariki na Kati (ECAPBA) ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya Viwango ya ECAPBA.
Kwa sasa Boniface Wamnura ni mwenyekiti wa Kamati ya Viwango ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC).
Akiwa mtaalam wa uandishi wa habari ambako amefanya kazi kama mwandishi mwandamizi na mhariri kweney vyombo mbalimbali vya habari, Wambura anategemea kuleta ujuzi wake wa mawasiliano kweney shirikisho hili linalokuwa kwa kasi sana katima ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na Kati.
Wambura anategemea kuongoza kamati ya watu watano (5) yenye jukumu la kuandaa na kuenndeleza orodha ya viwango vya mabondia toika nchi za Afrika ya Mashariki na Kati.
Baadhi ay wajumbe wanaounda Kamati ya Viwango ya ECAPBA ni pamoja na Simon Mukisa Katogole  wa Uganda na Steven Okumu toka Kenya.

SIMBA YAITUNGUA AZAM FC YA CHAMAZI MAGOLI 3-1 UWANJA WA TAIFA


Beki wa timu ya Simba Shomari Kapombe akimiliki mpira mbele ya Ibrahim Shikanda mshabuliaji wa timu ya Azam FC katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii jijini Dar es salaam, mpira umekwisha  Simba imeibuka  kwa ushindi mnono wa magoli 3-1 dhidi ya Azam FC ambayo yamefungwa na Felix Sunzu kwa kichwa na Emmanuel Okwi la pili na la tatu lililofungwa kipindi cha pili dakika za mwanzomwanzo, goli la Azam limefungwa na mshambuliaji John Boko.
Huko Arusha timu ya Yanga ilikuwa mgeni wa timu ya JKT Oljoro ya huko katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, ambapo Yanga imeibuka na ushindi wa goli moja lililofungwa na Mchezaji Mbuyu Twite
Wachezaji wa Simba wakishangilia mara baada ya kupata goli la pili katika mchezo huo.
Wachezaji wa timu aAzam FC wakisalimiana na wachezaji wa timu ya Simba kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Mashabiki wa timu ya Azam wakiishangilia timu yao wakati ikicheza na timu ya Simba uwanja wa Taifa jioni hii.Picha/Habari Na Full Shangwe Blog

JK ASHIRIKI MAZISHI YA MAREHEMU LUTENI KANALI MUSA MRISHO MTENGWA



 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya Marehemu Luteni Kanali Mussa Mrisho Mtengwa nyumbani kwa marehemu kijijini  Kiwangwa,wilayani Bagamoyo leo jioni wakati Rais Kikwete alipokwenda kushiriki mazishi ya Marehemu.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la marehemu Luteni Kanali Mussa Mrisho Mtengwa wakati wa mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu kijiji cha Kiwangwa wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani leo jioni.


Enzi za Uhai wake Marehemu Luteni Kanali Mtengwa aliwahi kuwa mpambe wa Rais wa awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi,kuanzia mwaka 1995 hadi mwaka 1995.Marehemu aliwahi pia kufanya kazi katika Wizara ya Sheria na kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya jeshi.

Marehemu alifariki juzi tarehe 25 Oktoba nyumbani kwake Kijitonyama
jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda na ameacha mjane, watoto wanne na wajukuu watatu Picha na Freddy Maro.

Saturday, October 27, 2012

BABYLOVE KALALA ANYAKUA TAJI LA REDDS MISS TANZANIA TALENT SHOW USIKU HUU

 
Mkurugenzi wa Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga akifungua rasmi shindano la Miss Tanzania Talent Show usiku huu  kwenye hoteli ya Girrafe Ocean View iliyoko kandokando ya bahari yaHindi jijini Dar es salaam, warembo wameonyesha vipaji vyao mbele ya watazamaji na wapenzi wa masuala ya urembo na usiku huu watapatikana watano watakaonigia kwenye ano bora na kutangazwa rasmi kwenye shindano la Miss Tanzania litakalofanyika Ubungo Novemba 3 mwaka huu , katika picha katikati ni Mbunge wa Arusha mjini viti maalum CCM Catherin Magige na kulia ni  Mkurugeni wa Hoteli ya Girrafe Ocean View Bwana Charles Bekon.
Fullshangwe inakumuvuzishia moja kwa moja matukio yanayoendelea kwenye show hii ya Miss Tanzania Talent Show kwenye hoteli ya Girrafe Ocean View  jijini Dar es salaam.
 
Mshindi wa Miss Tanzania Talent Show Babylove Kalala akicheza na nyika wakati wa shindano hilo lililofanyika usiku huu kwenye hoteli ya Girrafe Ocean View kandokando ya bahari ya hindi jijini Dar es salaam usiku huu.
Hawa  niyo walioingia tano bora ya shindano hilo lililofanyika usiku huu kwenye hoteli ya Gorrafe Ocean View jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Hoteli ya Girrafe Ocean View Bwana Charles Bekon akikaribisha wageni mbalimbali waliofika katika shindano hilo.
Miss World Tanzania Lisa Jensen kulia akiongoza majaji wa shindano hilo usiku huu kwenye hoteli ya Girrafe Ocean View usiku huu.
Wadau mbalimbali waliohudhuria katika show hiyo wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyojiri ukumbini hapo usiku huu mdau, mdau chini ni matukio mbalimbali ya show hiyo jionee mwenyewe mambo yaliyojiri kwenye hoteli hiyo usiku huu ni burudani na kushangweka kwa kwenda mbele kutoka kushoto ni Fredy, David na Isack.

RAIS WA ZANZIBAR DK ALI SHEIN AHUTUBIA BARAZA LA ELD EL HAJJ


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa,baada ya kupokea salamu ya Hesha ya gwaride la Kikosi cha Polisi FFU,leo alipowasili katika viwanja vya Salama Bwawani Hotel, akiwa mgeni rasmi kulihutubia Baraza la EID EL HAJJ Leo.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea salamu ya heshma ya kikosi cha polisi FFU,alipowasili katika viwanja vya Salama Bwawani Hotel,akiwa mgeni rasmi katika Baraza la EID EL HAJJ Leo.
 Baadhi ya askari wa Kikosi cha Polisi cha FFU wakitoa salamu ya heshma ya Gwaride kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,alipowasili katika viwanja vya Salama Bwawani Hotel, akiwa mgeni rasmi kulihutubia Baraza la EID EL HAJJ Leo
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi alipowasili katika Viwanja vya Salama Bwawani kuhutubia Baraza la EID El Hajj,lililofanyika leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, akisalimiana  na Viongozi na Kinamama baada ya kuwahutubia wananchi katika Baraza la Eid El Hajj. Leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar.
  Wananchi na waislamu wa Zanzibar ,wakike na wa kiume wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu katika baraza la Eid El Hajj,huko Ukumbi wa salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar leo.
  Baadhi ya Maw\aziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,yenye mfumo wa Umoja wa Kitaifa, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza na wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu katika baraza la Eid El Hajj,huko Ukumbi wa salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar leo.
   Wananchi na waislamu wa Zanzibar ,wakike na wakiume wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu katika baraza la Eid El Hajj, huko Ukumbi wa salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar leo.
  Mawaziri Wanawake wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye mfumo wa Umoja wa Kitaifa,wakimsikiliza Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu katika baraza la Eid El Hajj,huko Ukumbi wa salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar leo.
 Baadhi ya Wananchi na Waislamu wakijipatia vitafunio baada ya kumalizika Baraza la Eid El Hajj, lililohutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar Leo.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar

Worlds Mp’s insist for Parliamentary Immunities for better oversight


Delegation of Tanzania attending the panel session of the 127 Inter-Parliamentary Union Conference (IPU) during the discussion on Parliamentary Immunity: Benefit or Burden?. From Left is Hon. Suzan Lyimo (Mp), Mr. James Warbag, Assistant Director – Table Office and Hon. Hamad Rashid Mohamed (Mp).

Speaker of the National Assembly of Tanzania Hon. Anne Makinda poses for a group photo after the evening session of the conference with the delegation of Tanzania to the 127 Inter-Parliamentary Union Conference (IPU) in Quebec, Canada. From right is Hon. David Kafulila (Mp), Hon. Suzan Lyimo (Mp), Tanzania High Commissioner to Canada Hon. Alex Masinda, EALA Mp from Tanzania Hon. Dr. Perpetua  Nderakindo Kessy, and Mr. Joseph Sokoine Minister Plenipotentiary.Photo by Owen Mwandumbya
………………………………………………………….
By Owen Mwandumbya, Quebec Canada
Members of Parliament have spoken out in support of having immunities while performing the work as people’s representatives in parliaments and other works related to that. They said that during the Panel Session having a topic: Parliamentary Immunity: Benefit Or Burden? At the 127 inter- parliamentary Union (IPU) Conference which is taking place here in Quebec City, Canada since 21 to 26 October, 2012.
They said freedom of expression is the working tool of the Member of Parliament. It enabled them to do their jobs as representatives of people and to speak out criticize the government and denounce abuses. Parliamentary immunities is designed to ensure that parliamentarians can freely express themselves without hindrance and fear of prosecution.
During the debate, Mps said there is a tendency of Citizen generally to perceive immunity as a negative concept; they tend to see it as a way of politicians themselves to place above the law, thing that are very untrue.
This is particularly true in countries where parliamentary immunity, in the form of inviobility offers protections to Mps against legal proceedings for acts they carry it outside the confines of parliamentary duties.
The public reasoning they may be partly due to the lack of understanding of the purpose of parliamentary immunities. It may also reflect a more widely held belief that excessive parliamentary immunity offers protections to those who should be prosecuted and inversely failed to protect those who have done nothing wrong.
The panel discussion took place at the rationale and effectiveness of parliamentary immunity in today’s world in particular in  the light of public insistence on over greater accountability.
The main questions here were, should MPs enjoy parliamentary immunity, including from the legal proceeding for acts unrelated to parliamentary duties in order to effectively do their work? Should such immunity exist everywhere as a matter of principle or only in fragile democracies?
A parts from majority saying that immunities for Mps are inevitable, they also debate more on how can one ensure that application of parliamentary immunity indeed protects those subjected to political motivated charges – often members from the opposition and that inversely, the majority in parliament cannon block, for purely political reasons the prosecution of one of theirs.
Earlier, making his highlights, Mr. John Williams (Canada) CEO of the global organization of parliamentarians against corruption (GOPAC), urging that parliamentary immunity it is counter productive and outdated, drawing the recent decision by Slovak parliament to do away with the requirement of parliamentary authorization before a member a member of parliament can be prosecuted the point which was strongly opposed by many Mps and saying this is an irrelevant and does not freely gave the right of Mps to exercise the duties freely.
Sharing the experience from Tanzania, an Mp from Tanzania Hon. Hamad Rashid Mohamed said in Tanzania, statutory provisions covering parliamentary privilege is defined in Article 100 of the constitution of the United Republic of Tanzania, which covers the privilege of freedom of speech and debate in the Assembly and the parliamentary immunities, powers and privileges Act, 1988 (No.3 of 1988). 
The parliament and parliamentarians have the Immunity from legal proceedings which is clearly stated in the parliamentary immunities, powers and privileges Act, 1988 (No.3 of 1988) Section 5 which is provides as follows:- “No civil or criminal proceeding may be instituted against any member for words spoken before the Assembly or any of its Committees, or by reason of any matter or thing brought by him therein by petition, bill or motion or otherwise, or for words spoken or act done bonafide in pursuance of a decision or proceeding of the Assembly or a committee.’’

 Hon. Hamada also said that the law also provides the Immunity from arrest for civil debts which also the law in Section 6 of Act no. 3 of 1988 states as follows:- “No member shall be liable for arrest for any civil debt except for a debt the contraction of which constitutes a criminal offence.” One among the significant power the House has is the power of control over its own affairs and proceedings. This is one of the significant attributes of any independent Legislature.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI MSIKITI MPYA WA JIHAD WILAYA YA MWANGA-KILIMANJARO


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi katika Jengo la Msikiti mpya wa Jihad, baada ya kuzindua rasmi Msikiti huo uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro, leo Oktoba 26, 2012 wakati wa Sikukuu ya Eid El Hajj, iliyofanyika sambamba na uzinduzi wa Mfuko wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini wa Dini ya Kiislam katika Swala ya Idd El Hajj, iliyofanyika Kitaifa katika Msikiti mpya wa Jihad, uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro. Ibada hiyo ilifanyika sambamba na uzinduzi wa Msikiti huo na uwekaji wa Jiwe la Msingi pamoja na uzinduzi wa Mfuko wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre, leo Oktoba 26, 2012
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa Swala ya Idd El Hajj, iliyofanyika Kitaifa katika Msikiti mpya wa Jihad, uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro. Ibada hiyo ilifanyika sambamba na uzinduzi wa Msikiti huo na uwekaji wa Jiwe la Msingi pamoja na uzinduzi wa Mfuko wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre, 
leo Oktoba 26, 2012.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wananchi na waumini wa dini ya Kiislam, wakati akiondoka eneo hilo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na mmoja wa waumini wa Kiislam wa Kijiji cha Vuchama wakati akiondoka eneo hilo baada ya kuzindua na kuweka Jiwe la Msingi na kuchangisha fedha za ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre. leo Oktoba 26, 2012. Picha na OMR

RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAZI KWA MAWAZIRI NA MAAFISA WAANDAMIZI WA SERIKALI