Sunday, October 14, 2012

PICHA ZA MATUKIO YA UCHAGUZI WA CCM



 Baadhi ya wagombea wakaanza kujitoa katika kinyang'anyiro hicho jambo ambalo likaanza kuwagawa wapiga kura...Wagombea waliojitoa ni Bw.Juma Samwel Nkumba na Bw.Hajj Mlowezi Bagio.
  Wengine wakaanza kunong'onezana na kupashana habari kulikoni wagombea wawili wamejitoa?
 Bw.Salum Luzila diwani wa kata ya Tambukareli akiwa anatafakari kabla ya kuanza kupiga kura na tukio la wagombea wawili kujitoa!!!!
Mdau Bw.Yusuph Kitumbo akisikiliza kwa makini wagombea wakinadi sera zao katika uchaguzi huo.....Kitumbo naye ni mgombea wa nafasi ya Mwekahazina wa ccm mkoa wa Tabora.
 Bw.Yusuph Kitumbo akipiga kura kutekeleza haki yake ya msingi katika chama chake.
 Mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa mkoa Bw.Wakasuvi akijaribu kuwa karibu na mbunge mstaafu wa jimbo la Nzega Bw.Lucas Seleli
Mbunge wa jimbo la Igalula Dr.Athuman Mfutakamba akisalimiana na Bw.Yusuph Kitumbo wakati wa uchaguzi huo.
Mbunge wa jimbo la Nzega Dr.Hamisi Kigwangalla akiwa na baadhi ya wajumbe katika uchaguzi huo uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

No comments:

Post a Comment