Monday, October 15, 2012

WAASWA KUWA NA MAWAZO YA KUJIAJIRI WENYEWE


 Na Lucas Raphael,Tabora

WAHITIMU  wanaomaliza vyuo vikuu nchini wameaswa kutotengemea kazi za kuajiriwa na badala yake wawe na mawazo ya kujiajiri wenyewe.

Mkuu wa mkoa wa Tabora Fatuma Mwassa katika hotuba yake iliyosomwa na mkuun wa wilaya ya Tabora mjini Sulemani Kumchaya alisema kwamba lazima wahitimu wa vyuo vikuu kuondokana na mawazo ya kuajiriwa katika maisha yao .

Ameeleza ili kuondokana na mawzo hayo ya kuajiriwa ,wanafunzi wa vyuo vikuu ,ni lazima wae na mawazo ya kutumia elimu watakayopata kujiajiri tangu wanapoingia mwaka wa kwanza chuoni.

Akizungumza na wanafunzi wa chuo kikuu kishiriki cha Askofu mkuu mihayo (AMUCTA)katika kuukaribisha mwaka mpya wa masomu 2012 /2013.

Kumchaya amewahakikishia wanafunzi hao kuwa ofisi yake ipo tayari kuwasaidia ili wajiajiri pindi wamalizapo masomu yao katika chuo hicho kikuu .

Naye mwenyekiti wa bodi ya wakurungezi wa chuo hicho ,Askofu mkuu wa mhashamu Paul Ruzoka alisema kwambawananchuo kwa kuwepo kwao chuoni sio kujifunza kupata cheti bali kujingea ufanisi katika maisha yao na pia kuwasidia wengine na jamii kwa ujumla wake.

Askofu Ruzoka ambaye pia analiongoza jimbo kuu wa  la Tabora amewataka watumie fursa waliyoipata vizuri ,wakielewa kuwa serikali imewawezesha na jamii inawasubiri ili waitumikie .

Mwisho

No comments:

Post a Comment